Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 19, 2024 akiwa katika Mkutano wa hadhara Wilaya Temeke Jimbo la Mbagala ametoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya uhaba wa Sukari hapa nchini na jitahada za Serikali Chini ya kiongozi mahiri Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukabiliana na Changamoto hiyo.
RC Chalamila amesema si kweli hata kidogo kuwa Serikali haina majibu kuhusu uhaba wa Sukari pia sio sahihi kuwa Sukari haipatikani kwa sababu kuna wafanyabishara wameficha, ukweli ni kwamba katika Kipindi cha mwezi wa kumi na moja, kumi na mbili mwaka jana na mwezi wa kwanza mwaka huu viwanda vya ndani havikufanya uzalishaji wa Sukari
Sababu kubwa ya viwanda kutofanya uzalishaji hususani kiwanda cha Kilombero, mtibwa, kiwanda cha Moshi, Bagamoyo na Dakawa ni kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika mashamba ya miwa maji yalijaa na barabara ziliharibika kwa kiasi kikubwa ambapo hakuna magari yaliyoweza kuingia kwenye mashamba hayo.
Hivyo kutokana na kadhia hiyo uzalisha wa Sukari ulikuwa hafifu kwa kuwa miwa ikiwa katika hali nzuri tani 10 huweza kuzalisha Sukari tani 1 na miwa iliyoko kwenye maji tani 18 huweza kuzalisha Sukari tani 1.
Aidha RC Chalamila amefafanua kuwa kiwango cha Sukari ambacho kingekuwa toshelezi na ndicho kilichopangwa kwa nchi ya Tanzania ni tani 555,000 wakati kiwango cha sukari mwaka huu kilichopatikana ni tani 520,000 tu
Kwa kutambua Changamoto hiyo Serikali Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu iliamua kuagiza Sukari nje ya nchi, India na Brazil takribani tani 100,000 na Sukari hizo zinaingizwa hapa nchini pasipo kulipa kodi ya ushuru wa forodha pia bila kodi ya ongezeko la thamani hivi vyote vinafanywa na Serikali ikiwa ni jitihada za kukabiliana na uhaba wa Sukari hapa nchini.
Mwisho ni ukweli usio pingika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi mahiri wa Dkt Samia Suluhu Hassan ni Serikali sikivu " tusiwasikilize wapotoshwaji wasiolitakia mema Taifa letu" alisistiza RC Chalamila.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa