-Zaidi ya wanawake 600 katika wilaya zote tano za Mkoa wapatiwa sadaka ya IFTAR
-Awaomba kuendelea kuomba Dua kwa ajili ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 23,2025 ametoa Sadaka ya IFTAR kwa wanawake waisilam wa Mkoa huo zaidi ya 600 katika msikiti Mkuu wa Bakwata Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila ametoa Sadaka ya bidhaa mbalimbali kwa ajili ya IFTAR kama vile Mchele, mafuta ya kupikia, sukari, tende, Sembe na unga wa ngano kupitia kwa Mufti Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zuberi Bin Ally ambaye amepokea Sadaka hiyo na kuigawa kwa wanawake waislam wenye uhitaji wa Mkoa huo.
Aidha RC Chalamila akiongea wakati anatoa Sadaka kwa wanawake hao ametoa rai kuendelea kuomba Dua kwa ajili ya Mkoa na Taifa kwa ujumla vilevile tumuombee kiongozi wetu Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan. Pia " leo natoa Sadaka kwa kundi hili lakini ndani ya siku mbili zijazo nitafuturisha wana Dar es Salaam katika mazingira ambayo ni ya kawaida hivyo tutakualika tena Mufti Mkuu" . Alisema RC Chalamila
Kwa upande wa Mufti Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zuberi Bin Ally ameshukuru Mhe Albert Chalamila kwa upendo aliuonyesha kwa wanawake hao ambapo amesema neno pekee analoweza kusema ni Kumshukuru na Kumpongeza.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule na Mstahiki Meya wa Kinondoni Bwana Songoro Mnyonge kwa nyakati tofauti wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa Sadaka hiyo na wametoa rai kwa wananchi kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura zoezi ambalo linatarajiwa kuhitimishwa leo Machi 23,2025 kwa mujibu wa ratiba ya INEC
Mwisho " Na toeni katika vile tulivyokupeni kabla ya kufika mauti kwa mmoja wenu, akasema: Mola wangu Mlezi! Laiti ungenichelewesha muda mchache basi ningetoa sadaka na ningekuwa miongoni mwa wema." (Qura'an 63:10)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa