Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa mwezi mmoja kuanzia leo Julai 3, 2023 Wodi 3, ya watoto,wanaume na wanawake katika Hospitali ya Wilaya Kigamboni kukamilishwa na kuanza kutoa huduma.
RC Chalamila amesema hayo mapema leo wakati wa muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi katika Wilaya hiyo.
Aidha amemtaka mkandarasi anayejenga jengo hilo kurekebisha maeneo yenye mapungufu yote hususani zile sehemu zilizopinda huku akisisitiza lengo la *Mhe Rais Dkt Samia* ni kuona wananchi wa eneo hili wanapata huduma za afya katika hospali hii na tayari alishatoa fedha zaidi ya milioni 500.
Vilevile RC Chalamila amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kutengeneza Barabara za kuingia katika hospital hiyo kwa kutumia fedha za ndani angalao hata kwa kiwango cha changarawe na maeneo ya hospital hiyo yapandwe miti yenye faida kwa Afya ya mtoto na mgonjwa ambayo ni miti ya matunda pamoja na bustani za mboga mboga.
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Halima Bulembo* amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuyapokea maagizo na maelekezo yake na kwenda kuyafanyia kazi kwa wakati kwa masilahi mapana ya wananchi wa Kigamboni
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa