-Apongeza Halmshauri ya Temeke na Kigamboni kwa kupata hati safi
-Asema elimu ya kodi ifundishwe kuanzia kwa watoto wadogo
-Azitaka Halmshauri za Mkoa kubuni namna ya kukuza sekta ya Utalii
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 02,2024 ameshiriki Baraza maalum la Madiwani la Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG katika Halmshauri ya Manispaa ya Temeke Ukumbi wa Iddy Nyundo na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa nyakati tofauti.
RC Chalamila amewataka viongozi na watendeji wakati wote wanapotekeleza majukumu yao kuhakikisha wanaacha alama kwa kutekeleza miradi mikubwa ambayo ina masilahi mapana kwa wananchi kama vile ujenzi wa Hospitali kubwa, masoko ya kisasa, na maeneo ya vivutio vya utalii
Aidha RC Chalamila amepongeza wilaya ya Temeke kwa kupata Hati safi miaka 3 mfululizo pia Manispaa ya Kigamboni kwa kupata Hati safi miaka 7 mfululizo toka ianzishwe ambapo amewataka kuendeleza utamaduni huo pia kuhakikisha wanashirikiana na ofisi ya CAG, kuzingatia maelekezo na maagizo ya LAAC pamoja na ushauri wa mara kwa mara wa wakaguzi wa ndani
Vilevile amepongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato na kuwataka kuongeza kasi zaidi kwa kuwa na ubunifu wa kubuni vyanzo vipya na kubana mianya ya upotevu wa mapato lakini pia kuendelea kutoa elimu ya kodi hususani kwa watoto wadogo ili wakiwa watu wazima watambue kulipa kodi ni lazima na sio hiyari.
Sanajari na hilo RC Chalamila amesema bado Mkoa haujafanya vizuri katika sekta ya utalii ambayo ni fursa ya kuongeza mapato hivyo amewataka viongozi na watendaji kuketi kutazama upya sekta hiyo ambapo amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kusimamia hilo.
Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila alisema sio vema kuwa hodari wa kujibu hoja bali ni vizuri kuwa hodari katika kuzuia hoja kwa kuzingatia ushauri wa mkaguzi wa ndani lakini pia kuzingatia kanuni, miongozo na sheria za usimamizi wa fedha ili kuendelea kuweka historia ya kuwa na hati safi kila mwaka wa fedha kwa Halmashauri zote za Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa