Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 20, 2023 ametembelea shule ya msingi Olympio - Ilala Jijini la Dar es Salaam.
RC Chalamila amefanya ziara katika shule hiyo kwa lengo la kujionea uhalisia wa maendeleo ya shule hiyo katika nyanja za miundombinu, idadi ya wanafunzi, walimu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa ujumla wake
Akiwa shuleni hapo RC Chalamila ameelekeza Wazazi kulipa Ada ili kuiwezesha Shule hiyo kuboresha miundombinu na vitu vingine vinavyofanana na hivyo, pia ameagiza kuandaa kikao cha wazazi ambacho kitatoa fursa kwa pamoja kujadili mambo hayo huku akimtaka Mkurugenzi wa Jiji kwa kushirikiana na Mwl Mkuu kuandaa taarifa ya mapato na matumizi, taarifa ya madeni ya wanafunzi, hali halisi ya Taaluma, pia taarifa ya bodi ya shule.
Aidha RC Chalamila ameagiza kujengwa kwa ukuta wa mbele na nyuma na kufungwa camera kwa ajili ya usalama katika shule hiyo.
Sambamba na hilo Mhe Chalamila alipata wasaa wa kuongea na walimu kusikiliza Changamoto zao na kuzipatia majibu hata hivyo amewapongeza walimu kwa jitihada zao katika kufanya Kazi.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward mpogolo amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kutekeleza maagizo yake kwa wakati kwa masilahi mapana ya ustawi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Shule ya Msingi Olympio ni shule inayotumia lugha ya kingereza kufundishia na kujifunzia ina wanafunzi 5,567 walimu 67 wa Serikali na 23 wakujitolea
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa