Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Septemba 16, 2023 katika muendelezo wa ziara yake Wilaya ya Kinondoni ametembelea na kukagua athari za mazingira zinazotokana na Shughuli za kibinamu katika mto mpiji unaopakana kati ya Dar es Salaam na Pwani ambao ni mpaka kati ya mikoa hiyo miwili.
Akiwa katika ziara ya kukagua mto huo aliambatana na Kamati ya usalama, wadau wa Mazingira pamoja na wataalam wengine wakiwemo NEMC.
RC Chalamila alipata wasaa wa kusikiliza maoni mbalimbali kutoka kwa wadau na wataalam wa mazingira juu ya nini kifanyike ili kunusuru athari zinazoweza kujitokeza kutokana na uharibifu unaofanyika katika mto huo ambapo amemtaka kamanda wa polisi kulinda mto huo na kamwe wasikubali kutishiwa na mtu yeyote dola lazima ipewe heshima yake.
Aidha RC Chalamila amesema katika kulinda mto huo lazima kuwe na uratibu wa pamoja hivyo anaendelea kukusanya taarifa za kitaalam na atarudi tena "modal" nzurii yenye kuleta namna bora ya kulinda mto huo kwa masilahi mapana ya Umma.
Vilevile Mhe Saad Mtambule Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amesema wako tayari kushirikiana na Wilaya jirani ya Bagamoyo kuja na mkakati wa pamoja katika kuona namna bora ya kuhifadhi mto huo wako watu watu wana chimba mchanga pasipo kufuata taratibu za uchimbaji.
Mwisho Mhe Albert Chalamila alifika katika daraja linalotenganisha mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ukielekea Bagamoyo ili kujionea uhalisia hususani kutokana na uwezekano wa kunyesha mvua kubwa kama mamlaka ya hali ya hewa ilivyotabili na hatua gani za haraka zinaweza kuchukualiwa endapo mvua hizo zitanyesha
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa