Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 11,2023 ametembelea maonesho ya Sabasaba ya Kimataifa 2023 katika viwanja vya Mwl JK Nyerere Temeke Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu na Dkt Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa ambapo wameweza kusimamia viwanda vya ndani ambavyo vinazalisha bidhaa nyingi zinazouzwa katika masoko ya ndani na nje hili ni jukumu kubwa sana ambalo sisi kama watumishi tunapaswa kuliendeleza kwa kiasi kikubwa ili mwisho wa siku Tanzania iweze kujulikana kimataifa.
Aidha RC Chalamila amefurahishwa na bidhaa mbalimbali zinazouzwa na wafanyabishara wa aina mbalimbali, wadogo, wa kati na wakubwa huku akiwataka watanzania ambao bado hawajafika katika viwanja hivyo kuja kujipatia bidhaa na kujionea fursa anuai kwani maonesho ya 47 yameboreshwa sana.
Aidha Mhe Chalamila amesema kupitia wafanyabishara walioko katika viwanja hivyo vya maonesho yanaleta picha ya Kimataifa, Kitaifa na ngazi ya chini kabisa ya Wajasiriamali ambao ni wanufaika wa mikopo ya 10% inayotolewa na Serikali ya Rais Dkt Samia.
RC Chalamila pia amewataka wafanyabishara kuendelea kufanya biashara na kuwahakikishia ulinzi na usalama upo wa kutosha pia muda wa kufanya biashara umeongezwa hadi saa 2 usiku.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE Bi Latifa Khamis amemshukuru Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila kwa kufanya ziara katika hiyo na usimamizi wake katika Kipindi chote cha maandalizi ya maonesho pia ulinzi na usalama umeimarika hata hivyo ujio wake umewafariji wananchi na wafanyabishara wa ndani na nje kwa kuwa wanaona Serikali inavyounga mkono maonesho hayo, vile vile wafanyabishara wameendelea kufanya biashara vizuri, hivyo ametoa rai kwa wananchi walioko majumbani kuja kujipatia bidhaa mbalimbali katika maonesho hayo ya Kimataifa ya 47
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa