Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 17,2023 ametembelea maeneo ya kimkakati katika Bandari ya Dar es Salaam (TPA) akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa huo.
RC Chalamila akiwa katika Bandari hiyo amepata wasaa wa kusikiliza taarifa fupi ya uendeshaji wa Bandari na kisha kwenda kujionea *miundo mbinu na mitambo katika Bandari hiyo kuanzia Gati namba O hadi 7
Aidha Mhe Chalamila amemshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake njema ya kuboresha Bandari ili ilete tija kwa masilahi mapana ya Taifa huku akiwataka watanzania kuachana na upotoshwaji unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa letu
Mhe Chalamila amejionea Gati namba 0 inayohudumia magari, Gati namba 1-4 mizigo, Gati namba 5-7 makasha ambapo teknolojia inayotumika haikidhi viwango vya Kimataifa kuna mitambo miwili tu ya kisasa (SSG) ambayo Mhe Rais amenunua na haitoshelezi inahitajika zaidi ya 50 hivyo ni lazima kushirikisha sekta binafsi.
Hata hivyo RC Chalamila ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Bandari kuendelea kuwaalika watu wa aina mbalimbali hususani wanasiasa ili wapate uelewa wa uendeshaji wa Bandari hiyo, pia wanasheria wa Bandari kuendelea kufafanua vipengele vya makubaliano kati ya TPA na DP world ili watu waelewe dhamira njema ya Rais, Taifa linahitaji kusimama imara lazima tumuunge mkono Rais aendelee kusonga mbele.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa TPA Ndg Mrisho Selemani amesema pamoja na makubaliano ya TPA na DP world suala la ulinzi na usalama ni la Bandari kama ilivyo sasa wananchi waondoe hofu pia ili Bandari iweze kufikia viwango vya Kimataifa lazima maboresho makubwa ya teknolojia ya kisasa na miundo mbinu yafanyike, kufikia hatua hiyo uwekezaji mkubwa unahitajika tena kwa gharama kubwa, hivyo kufanikiwa hilo ni lazima Serikali ishirikishe sekta binafsi "kwa mfano maboresho ya Gati moja ni zaidi ya Dola za kimarekani million 100" Alisema Ndg Selemani hivyo makubaliano ya Uendelezaji Bandari ya DSM na DP world ni fursa adhimu ambayo inapaswa kuungwa mkono kwa masilahi mapana ya Taifa na Ustawi wa jamii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa