Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Decemba 07,2023 ametembelea na kukagua mali na mitambo ya kiwanda cha chibuku kilichoko Ubungo ambacho kwa muda mrefu kimesimama uzalishaji wa pombe hiyo.
RC Chalamila akiwa katika eneo la kiwanda amesema ujio wake katika kiwanda hicho ni kujionea mali zilizoko kwa ajili ya kukabidhi rasmi kiwanda pamoja na mali zote kwa Halmashauri tatu ambazo ni Jiji, Temeke na Kinondoni, Halmashauri hizo tatu zitakabidhiwa kiwanda hicho na TBL kwa mujibu wa Sheria.
Aidha RC Chalamila amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi Rehema Madenge kuunda timu ya makabidhiano ndani ya muda mfupi, na baadaye iundwe bodi ya mpito ambayo itafanya kazi hadi pale Bodi rasmi itakapo undwa
Vilevile RC Chalamila ameelekeza wakati wote wa vikao muwakilishi kutoka Wilaya ya Ubungo na Kigamboni awepo na ashiriki vikao hivyo " baada ya kiwanda hicho kukabidhiwa kwa Halmashauri hizo 3 ndipo namna ya uendeshaji, uzalishaji wa kinywaji gani utajulikana" Alisema RC Chalamila
Sambamba na hilo RC Chalamila amesema dhamira ya kufufua kiwanda hicho ni kutekeleza maagizo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kiwanda hicho kitafungua fursa za ajira kwa jamii pia Serikali itapata mapato " kukiacha kiwanda hicho kikiwa haikifanyi kazi Serikali inapoteza mapato mengi pamoja na kupoteza fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania kitu ambacho hakikubaliki hata kidogo" Alisisitiza Mhe Chalamila
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa