-Amtaka Naibu kamishna wa Ardhi Mkoa kuanza utaratibu wa kupima mara moja.
-Aagiza waliofoji nyaraka wachukuliwe hatua Kali za kisheria
-Awataka wenyeviti na Watendaji wa kata na mitaa kutokuwa sehemu ya migogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametangaza rasmi eneo la Muhimbili-Pemba Mnazi Wilaya ya Kigamboni kuwa chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia leo Mei 17, 2024.
RC Chalamila ameyasema hayo leo Mei 17,2024 akiwa katika eneo hilo ambapo alisema " tumepitia nyaraka zote tumejiridhisha hakuna mwenye umiliki halali wa eneo hilo" Alisema RC Chalamila
Aidha RC Chalamila amesema wale wote waliofoji nyaraka kwa kujifanya ndio wamiliki wa eneo hilo hatua kali zichukuliwe, vilevile amemtaka Naibu kamishna kuanza utaratibu wa kupima maeneo hayo na Wananchi wenye uhitaji wa Ardhi watafuata taratibu za kuomba kununua maeneo hayo pia ameelekeza Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Wananchi kusimamia ulinzi na usalama wakati wate wa zoezi hilo
Pia amewataka wenyeviti na Watendaji kutokuwa sehemu ya migogoro katika maeneo yao badala yake waiwakilishe Serikali vizuri " Unakuta Mwananchi ananunua kipande cha Ardhi mwenyekiti au mtendaji anathibitisha kuwa hakina mgogoro baada ya siku chache anamuambia kina mgogoro wakati tayari ameshatoa pesa acheni hiyo tabia" Alisema RC Chalamila
Kwa upande wa mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi kutoka Ofisi ya Naibu kamishna wa Ardhi Mkoa Bwana Costa Chaula amesema baada ya uchunguzi waliweza kubaini watu sita tofauti ambao walijifanya kuwa ni wamiliki lakini baada ya kufutilia nyaraka zao zimeonekana kuwa na mapungufu kiasi cha kushindwa kuthibitisha uhalali wao kumiliki eneo hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa