Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameutaka uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kusimamia vema mchakato wa upatikanaji wa Viongozi waadilifu wa soko hilo ili kukabiliana na kasoro zilizoko hivi sasa.
RC Chalamila amesema hayo leo Agosti 16, 2023 alipo zuru katika Soko hilo kukagua miundombinu na kuongea na wafanyabishara wa Soko hilo
Mhe Mkuu wa Mkoa amebaini kasoro mbalimbali ikiwemo Usalama hafifu wa Soko, Upangishaji holela ambapo wako baadhi ya watu wasiowaaminifu hupangisha meza kwa bei ya juu inayokizana na bei halisi ya Serikali pia uwepo wa miundombinu chakavu ndani ya Soko.
Hata hivyo RC Chalamila amekemea uwepo wa madalali katika Soko ambao hupandisha bei za Upangishaji wa fremu na meza, kuepuka rushwa, pia kuimarisha ulinzi shirikishi, na usafi wa Soko pamoja na Viongozi wa mwanzo kutogombea tena nafasi za uongozi katika Soko hilo wapishe Viongozi wapya.
Aidha RC Chalamila ameagiza TAKUKURU kuwakamata wale wote wanaohusika na uuzaji wa meza kwa bei ya juu wahojiwe wakikutwa na hatia wapelekwe mahakamani, pia amewahakikishia wafanyabishara hao kuzimaliza Changamoto zote katika Soko hilo kwa Kipindi kifupi.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amesema soko hilo lina wafanyabishara takribani 883 dhamira ya Manispaa ni kuboresha Soko hilo, kupata uongozi imara wenye kutetea masilahi ya wafanyabishara ndio maana tuliamua kuvunja uongozi wa mwanzo na sasa tuko katika Kipindi cha mpito kupata uongozi mpya wa Soko
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa