Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema Katika kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa mazingira Serikali ya Mkoa huo imekusudia kutoa mitungi ya gesi kwa wanawake miatatu (300) kwenye kila wilaya mkoani humo ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi na kuepuka ukataji miti
RC Chalamila amezungumza hayo Juni 5,2024 Jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yaliyofanyika kimkoa wilayani kigamboni katika viwanja vya Mji mwema.
Mhe Albert Chalamila amesema matumizi ya nishati safi ndio nyenzo muhimu ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira hasa ukataji miti hivyo mpango huo wa kugawa mitungi ya gesi utatoa hamasa ya utumiaji nishati safi
Aidha RC Chalamila amewataka wasimamizi wa misitu kusimamia vyema sheria za misitu ili kuepuka ukataji miti badala ya kusumbuka na wauza mkaa kwani mkaa hupatikana baada ya miti kukatwa hivyo nguvu kubwa ielekezwe kwenye kuzuia ukataji miti
Aidha Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema Rais Dkt Samia ambaye ni kinara wa Nishati safi katika utunzaji mazingira ameonesha njia na nia njema ya kutunza mazingira hivyo ni muhimu kumuunga mkono kwa vitendo
Kwa upande wake Meneja wa baraza la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC kanda ya Temeke Anord Mapinduzi amesema siku ya mazingira duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo juni tano kufuatia shughuli za maendeleo kuanza kuathiri mazingira ambapo ilionekana ni muhimu kuikumbusha jamii kutunza mazingira hivyo amesisitiza wadau wote kuendelea kuungana kutunza mazingira kwa vitendo
Naye Capteni Rosimery David Katani Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya usafi ya SUMA JKT mmoja wa wadau wakubwa wa mazingira aliepatiwa tuzo ya utunzaji wa mazingira ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali kwenye utunzaji wq mazingira kwa kuhakikisha anasimamia vyema usafi wa mazingira
Sanjari na hayo RC Chalamila amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila kukaa na wakurugenzi wa Halmashauri kuangalia namna bora ya kuboresha miundombinu ya Dampo la Pugu pamoja na kuja na mikakati ya kurejeresha taka kupitia wasomi walioko na wawekezaji.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali, mamia ya wananchi, Kamati ya usalama ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila pamoja na mambo mengine maadhimisho hayo pia yalienda sambamba na utoaji wa tuzo kwa wana mazingira bora vilevile yamebeba kauli mbiu isemayo "Urejeshaji wa ardhi kupambana na hali ya jangwa na ustahamilivu wa ukame"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa