-Asema nchi za Afrika zina kila kitu lakini bado hazijawekeza vizuri katika mtaji wa kibinadamu (Human Capital).
-Awataka wazazi na walimu kuwawezesha wanafunzi kutambua uwezo wao kama wanajamii wenye tija.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 18, 2024 akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita St Joseph Cathedral, amezitaka Taasisi za elimu ikiwemo shule za Sekondari kujipanga vizuri katika kuandaa mtaji wa kibinadamu (Human Capital) wa badaye.
RC Chalamila amesema hayo leo wakati wa mahafali ya 13 ya kidato cha sita 2024 katika shule ya St Joseph Cathedral inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam.
Mhe Albert Chalamila amesema mtaji wa kibinadamu (Human Capital) unajumuisha maarifa, ujuzi, na Afya ambayo watu huwekeza na kujilimbikiza katika maisha yao yote na kuwezesha kutambua uwezo wao kama wanajamii wenye tija.
Aidha RC Chalamila amesistiza mtaji huo wa kibinadamu uwekezaji wake unaanza katika ngazi ambazo vijana hupatiwa elimu kama ilivyo katika shule hii ya St Joseph Cathedral.
Sanjari na hilo RC Chalamila alishiriki kutoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri pia aliendesha harambee kwa wazazi na wageni waalikwa ili kutoa zawadi kwa Mkuu wa Shule, vilevile ameikabidhi shule hiyo pikipiki mpya kwa ajili ya matumizi madogo madogo shuleni hapo
Mwisho Mhe Albert Chalamila amewataka wazazi na walimu kuwawezesha wanafunzi kutambua uwezo wao kama wanajamii wenye tija " Tuache kuwalinda sana watoto lazima tuwajenge katika mazingira ya kutambua siku moja watakua na maisha yao na watatakiwa kutoa mchango kwa Taifa lao pasipo kumtegemea Mzazi kwa masilahi mapana ya Taifa" Alisema RC Chalamila
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa