Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi katika jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali, katika ukumbi wa Maktaba Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) leo Julai 28, 2023
RC Chalamila amesema anatambua mchango wa mashirika yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo na ustawi wa jamii ya Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla ambapo amewataka kuwekeza katika Rasilimali watu ili kuweza kupiga hatua zaidi.
Aidha Mhe Chalamila amezitaka NGOs kuakisi maadili ya kitanzania, kuhamasisha uzalendo, kutoa elimu ya utambuzi wa haki za binadamu na uwajibikaji pia kujenga misingi imara ya kujitegemea kiuchumi na kuwasilisha taarifa mbalimbali ikiwemo taarifa za robo za utekelezaji wa majukumu yao.
Hata hivyo RC Chalamila amesema Mkoa wa Dar es Salaam una maeneo mengi ambayo mashirika hayo yakishiriki ipasavyo Mkoa utasonga mbele kimaendeleo mfano Mazingira nyanja ya taka, na mipango miji nyaja ya ujenzi holela, pia ametoa rai kuelekea Kipindi cha uchaguzi mashirika hayo yajikite kutoa elimu ya uchaguzi na si vinginevyo.
Vilevile Mhe RC Chalamila amepokea maombi maalum yaliyowasilishwa kwake na jukwaa hilo ikiwemo Ofisi yake na Halmashauri kutenga bajeti, kuendelea kushirikiana na majukwaa hayo, kusaidia kushawishi mabadiliko ya sera za kodi zinazotozwa kwa NGOs na kuwa balozi katika kuelezea umuhimu wa mashirika hayo kwa jamii.
Mwisho Jukwa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Dar es Salaam 2023 lenye kauli mbiu " Mashirika yetu, Maadili yetu,Taifa letu" limejadili mada mbalimbali ikiwemo Changamoto na mapendekezo ya kodi nchini, Changamoto na uzingatiaji wa sheria za usimamizi na uendelezaji wa NGOs pia mwelekeo na nafasi NGOs kukabiliana na Changamoto za uendelevu zilizopo na zijazo kitaifa na kimataifa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa