- Asema mchakato wa Jambo hilo umefuata taratibu zote hitajika
- Imedhihirika kuwa Kigamboni kwa sasa Kuna idadi kubwa ya watu
- Asema hii itasaidia kupanua Maeneo ya Kiutawala
- Wajumbe wote wa Kikao hicho wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni wafurahia kuungwa mkono kwa hoja hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Novemba 29, 2023 ameridhia ombi la kugawa maeneo ya Kiutawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Kama yalivyowasilishwa
Mhe. Chalamila amesema mchakato huo umefuata hatua zote stahiki ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo husika na kutembelea wananchi na viongozi Kisha kufanya mahojiano nao
Hata hivyo, RC Chalamila Amepokea maoni mbalimbali ya Wajumbe hao ambapo kwa Umoja wao wamedhihirisha kuwa Kigamboni kwa sasa Ina ongezeko kubwa la watu wanaohamia kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu
Vile vile Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema utekelezaji wa Jambo hili utasaidia kupanua Maeneo ya kiutawala ya Kigamboni ambapo wananchi watapunguziwa umbali wa kwenda kupata huduma mbalimbali
-Kwa upande wa Wajumbe wote wa kikao hicho wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya wamefurahishwa na kupitishwa kwa mapendekezo ya kugawa baadhi ya kata na mitaa ya Kigamboni
Ikumbukwe kuwa Halmashauri hiyo kutokana na ukubwa wake na uhamiaji wa watu halmashauri hiyo imeona ni vema kuongeza idada ya kata kutoka 9 hadi kata 14 na Mitaa 67 hadi 77 ikiwa ni ongezeko la Kata 5 na Mitaa 10
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa