Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 5,2024 amepkea ugeni kutoka Comoro ambao wamekuja kwa lengo la kuimarisha mahusiano katika nyanja mbalimbli kati ya Tanzania na Comoro hususani jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Akiongea na ujumbe huo kutoka Comoro RC Chalamila amesema ujio wa ugeni huo ni matunda ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambayo amekuwa akiyafanya kwa mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo Comoro ambapo amendeleza mahusiano na taifa hilo ambayo yalikuwepo toka enzi za utawala wa Baba wa Taifa Mwl JK Nyere hivyo amewahakikishia Mkoa wa Dar es Salaam uko tayari katika mashirikiano na Comoro kwa masilahi mapana ya nchi zote mbili
Aidha RC Chalamila amesema Mkoa huo una fursa nyingi ikiwemo idadi kubwa ya watu, Bandari, Uwanja wa kimataifa wa ndege na miundombinu mingine mingi ya kisasa ikiwemo reli ya kisasa SGR.
Sanjari na hilo amesema kwa kuwa dhamira ya serikali ya awamu ya sita ni kuvutia wawekezaji chini ya uongozi wake amewahakikshia mazingira Rafiki katika kila nyanja ambayo wataona inafaa kufanya mashirikiano au kuwekeza.
Mwisho wakati wa mazungumzo hayo mhe Mkuu wa Mkoa aliambatana na Waheshimiwa Mameya wa Halmashauri za Mkoa huo,wataalam kutoka ofisi yake wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo DKT Toba Nguvila.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa