-Mwenge wa Uhuru DSM utakimbizwa katika umbali wa KM 499.9
-Miradi 32 yenye thamani ya Tsh 93,457,467,363.83 kupitiwa na Mwenge wa Uhuru
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 24,2023 amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoa wa Pwani katika viwanja vya Tazara -Temeke Jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa mapokezi ya Mwenge huo RC Chalamila amesema Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam utakimbizwa katika umbali wa KM 499.9 kwa kupitia miradi 32 yenye thamani ya Shilingi Bilioni Tisini na Tatu, Milioni Mianne Hamsini na Saba Laki Nne na Elfu sitini na Saba, Mia Tatu Sitini na Nane na Senti Themanini na Tatu (93,457,467,363,.83)
Aidha RC Chalamila amesema miradi hiyo ipo iliyokamilika na mingine ipo katika hatua mbalimbali za Utekelezaji
Mhe Albert Chalamila amekabidhi mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya Temeke ambayo ndiyo Wilaya ya Kwanza kukimbiza Mwenge huo katika Mkoa huo, ambapo Tarehe 25/05/2023 utakabidhiwa Wilaya ya Kigamboni, Tarehe 26/05/2023 Wilaya ya Ilala, Tarehe 27/05/203 Wilaya ya Ubungo na Tarehe 28/05/2023 Wilaya ya Kinondoni na baadae utakabidhiwa *Mkoa wa Kusini Magharibi - Zanzibar.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 unachagizwa na kauli mbiu ya " *Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa* "
# *Karibu Mwenge wa Uhuru Dar es Salaam, Kazi Iendelee
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa