-Aishukuru Kampuni ya Doweicare na kuiomba kuendelea kuisaidia Hospital ya Muhimbili katika maeneo mengine yenye uhitaji
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 22,2024 amepokea msaada wa diapers kutoka Kampuni ya Doweicare na kukabidhi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya milioni 35 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Akipokea msaada huo wa diapers aina ya soft care ambazo zinazalishwa na Kampuni ya Doweicare ameishuru Kampuni hiyo kwa kugusa maisha ya watoto ambao wanajifungua katika hospital hiyo ambapo ameiomba Kampuni hiyo kuendelea kuisaidia hospitali hiyo ya Taifa katika maeneo mengine ili kuunga mkono Juhudi za Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika Kuboresha Sekta ya Afya hapa nchini.
Aidha RC Chalamila ametoa rai kwa makampuni na wadau wengine kutoa misaada katika sekta mbalimbali zinazogusa jamii moja kwa moja kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii.
Kwa upande Zari ambaye ni balozi wa bidhaa hiyo ya softcare amesema yeye ni mwanamke hivyo amekuwa akiguswa sana kuona baadhi ya wazazi wakijifungua na kutokana na ugumu wa maisha kukosa baadhi ya huduma muhimu hivyo ameiomba Kampuni hiyo ambayo amekuwa akifanya nayo kazi kwa muda mrefu kuwasaidia
Mwisho msaada huo umekabidhiwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akiwa na wataalam wengine wa hospitali hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa