Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 24,2025 ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa Elika Nasson Nguvila ambaye ni Dada wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila katika kanisa la KKKT Bombambili Ukonga Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila akiongea wakati wa kuaga mwili wa Elika Nguvila amesema kifo ni mpango wa mwenyezi Mungu " Ukisoma vitabu mbalimbali viko vinavyoeleza miaka ya mwadamu kuishi ni 70 na vingine vinasema miaka 120 katika kipindi chote cha uhai wa binadamu tukumbuke kutendeana mema dunia ni mzunguko na watu ni walewale".Alisema Chalamila
Aidha RC Chalamila ameahidi kuchangisha shilingi milioni 7 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa ushirika huo ambapo yeye binafsi ameahidi kutoa milioni 2 vilevile ametolea ufafanuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi eneo hilo ikiwemo barabara ambapo amesema Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan itazimaliza changamoto hiyo kwa sasa tayari wakandarasi wameshalipwa kuanza ujenzi wa barabara ya Kivule kwenda msongola na barabara zingine zitafuata awamu ijayo.
Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Elias Mpanda ametoa pole kwa wafiwa kufuatia msiba huo ambapo amesema anaungana na Mkuu wa Mkoa kuchangia milioni moja papo hapo kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na kuhusu changamoto za barabara amewahakikishia Serikali itazifanyia kazi kama alivyosema Mkuu wa Mkoa.
Mwisho mwili wa marehemu Elika unasafirishwa leo kuelekea Makete Mkoa wa Njombe kwa ajili ya Maziko
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa