-Amtaja Rais Dkt Samia kuwa shujaa aliye hai kutokana na kazi kubwa anayoifanya ndani ya Taifa hili.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 25,2024 ameongoza viongozi na mamia ya wananchi wa Mkoa huo katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa wa Tanzania katika eneo la Mnara wa Mashujaa Mnazi mmoja Ilala Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amewataka wakazi wa Mkoa huo na watanzania kwa ujumla kuwaenzi mashujaa kwa kuendelea kudumisha Amani ya nchi ambapo amesema wako mashujaa walioipigania nchi hii walishatangulia mbele ya haki na wapo mashuja walio hai mfano mzuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ni shujaa aliye hai kupitia kazi nzuri anayoifanya ndani ya Taifa hili ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika jamii kama vile SGR, Bwawa la Mwl Nyerere na miradi mingine mingi ya Elimu na Afya.
Aidha RC Chalamila amesema siku ya mashujaa ina umuhimu mkubwa katika historia ya Tanzania na kusema kuwa njia bora ya kuwaenzi mashujaa hao ni kuendelea kudumisha Amani na kuepuka viashiria vyote vya uvunjifu wa Amani
Sanjari na hilo RC Chalamila amesema Tanzania imepitia majaribu mengi kabla ya kupatikana kwa Uhuru na amani iliyopo sasa na kueleza kuwa Amani iliyopo ni matokeo ya kazi nzuri iliiyofanywa na mashujaa waliopoteza maisha pamoja na mashujaa waliohai ambao ni viongozi waliojitoa kuilinda na kusimamia amani ya nchi , hivyo ni muhimu kila mtu kuilinda amani.
Ifahamike kuwa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa Kitaifa yamefanyika katika Mkoa wa Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani ameongoza maadhimisho hayo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa