Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 5,2024 ameongoza kikao cha kisheria cha kamati ya ushauri ya Mkoa(RCC) ambacho pamoja na mambo mengine kimejadili taarifa ya utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2022/2023, 2023/2024 na pendekezo la mpango wa Bajeti ya mwaka 2024/2025
Vilevile kupitia kikao hicho maadhimio mbalimbali yameadhimiwa ikiwemo mchakato wa kuanzishwa kwa mfuko maalum wa barabara wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuunda kamati maalum ya kupitia muundo wa Jiji la DSM, na Kupitisha Bajeti iliyojadiliwa kwa kishindo.
Aidha RC Chalamila amewataka viongozi na Wataalam katika Mkoa huo kufikiri kwa ukubwa wake jambo lolote la kimaendeleo kwa kuwa Mkoa huo ni tofauti kabisa na mikoa mingine ya Tanzania kila kinachofnayika ni vizuri kifanyike tofauti kama ni ujenzi wa masoko, tufikiri tofauti Alisema RC Chalamila
Vilevile Mkuu wa Mkoa amesema ni wakati muafaka wa kuanza kufanya kazi saa 24 ambapo amepongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri ya kusimamia ulinzi na usalama katika Mkoa Hali ni shwari kutokana na kazi nzurii ya jeshi hilo.
Sambamba na hilo RC Chalamila amesema hivi karibuni Soko la Karia Koo litafunguliwa rasmi na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kifungua soko hilo, hivyo ameelekeza viongozi wa Wilaya kuendelea kuwapanga vizuri wafanyabishara wadogo na kuendelea kusafisha na Kupendezesha mazingira mbalimbali ya Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa