-Asema ajaridhishwa na mwenendo wa kazi, kwa kuwa mpaka sasa haoni vifaa vyovyote eneo la mradi.
-Asisitiza wananchi wa Kitunda, Kivule, Msongola na majohe njia 4 wanataka kuona barabara za lami sio vinginevyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 24, 2025 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kitunda, Kivule Msongola na Majohe njia 4 ambayo toka makataba wa ujenzi usainiwe mwaka jana mpaka sasa Mkandarasi amejenga Camp tu na vifaa vya ujenzi havionekani licha ya kuwa alishalipwa sehemu ya fedha za kuanza ujenzi huo.
RC Chalamila amemtaka Mkandarasi kuanza ujenzi huo mara moja, atakapokuja tena aone mabadiliko makubwa la sivyo hatakuwa na uvumilivu tena vilevile amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kumuandalia Mkutano wa hadhara ili aweze kuongea na wananchi wamueleze kero zao. "Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo barabara ili kuwa na jamii yenye ustawi hivyo wakazi wa eneo hilo wakae mkao wa kula" Alisema Chalamila.
Vilevile RC Chalamila amesisitiza Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni wa kipekee kila kitu kihitaji pesa na ili upate pesa lazima uhangaike muda wote na kuhangaika kunahitaji amani hivyo kila mmoja ana kila sababu ya kuilinda amani kwa nguvu zote.
Naye Meneja TARURA Mkoa Mhandisi Jofrey Mkinga amesema kwa mujibu wa mkataba Mkandarasi huyo mpaka sasa yuko nje ya muda kwa miezi miwili kitu ambacho amekifanya eneo la mradi hadi sasa ni kujenga Camp tu hivyo utekelezaji wa mradi uko chini.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa hufanya ziara katika Wilaya hiyo ambapo amesema changamoto za wakazi wa eneo hilo ilikuwa ni barabara pamoja Vituo vya Afya hivyo anamuomba Mkuu wa Mkoa kumpelekea salaam za wana Ilala Mhe Rais kwa kutoa pesa za ujenzi wa barabara na kituo cha afya ambacho ujenzi wake unaendelea.
Mwisho mwenyekiti wa Mtaa wa Mbondole Bwana Thomas Nyanduli amesema anajisikia furaha kuona mkuu wa Mkoa amekuja kukagua mradi huo hivyo ameshukuru na kupongeza kwa dhati kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na walioko chini yake hususani Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa