Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo April 22, 2024 amekutana na wafanyabishara wanaomiliki viwanda vya saruji na Nondo ambavyo ni MMI, LAKE, CAMEL, TWIGA na KIBOKO katika Mkoa huo Ofisini kwake Ilala Boma.
Akiongea na wamiliki hao wa Viwanda vya Saruji na nondo amesema amewaita kwa lengo la kufahamiana vilevile na wao kupata fursa ya kuwafahamu viongozi wao ngazi ya Mkoa ili pale kunapokuwa na changamo wajue nani wakuweza kutatua kwa masilahi mapana ya mkoa na Taifa kwa ujumla.
Aidha RC Chalamila amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anathamini uwekezaji hapa nchini ndio maana siku zote amekuwa akiboresha mazingira ya wawekezaji ambapo ameweza kuunda wizara maalum ya uwekezaji na Mipango hiyo yote ni katika jitihada za kuimarisha uwekezaji na kuvitia wawekezaji.
"Na sisi ambao tuko chini yake katika maeneo yetu jukumu letu kubwa ni kuhakikisha tunaweka mazingira mazuri na rafiki kwa wawekezaji ili kwenda sambamba na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu.
Sambamba na hilo RC Chalamila amesema atanya ziara katika viwanda hivyo ili kuweza kujua Changamoto zinazowakabili pamoja na kuwatia moyo katika uwekezaji wao lakini pia amewaomba kuwa marafiki wazuri wa Serikali, walipe kodi bila shuruti na kuwa mabalozi wazuri bila kusahau kuchangia maendeleo ya Mkoa ikiwemo ujenzi wa hosteli za kike ili kuondoa adha inayowakabili wanafunzi katika Mkoa huo.
Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila amewataka wafanyabishara hao kuchangia maendeleo ya Mkoa huo hususani ujenzi wa hosteli kwa kuwa wanafunzi wa mkoa huo wamekuwa wakipata shida za usafiri, mimba ambavyo vinapelekea kushusha viwango vya ufaulu wa katika masomo yao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa