Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila leo Desemba 19,2023 amekutana na wamiliki wa Bars, Night Clubs na Grocery katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga Jijini humo
Akiongea na wamiliki hao RC Chalamila amesema maeneo hayo ya starehe yanabeba watu wengi ni fursa kubwa ya ajira kwa vijana na husaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla lakini pia ni hatari kama biashara zitaendeshwa pasipo kuzingatia misingi ya amani, hivyo ni vizuri kujiepushe kuwa vichaka vya waovu, vibaka na majambazi hivyo ni wajibu wetu sote kumuunga mkono Mhe Rais Dkt Samia S. Hassan kwa kulipa kodi bila shuruti kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi na watu wake.
RC Chalamila alisema tunaelekea kwenye sikukuu hivyo amani ni jambo lakuzingatia zaidi, "Kwakuwa ninyi ni wadau wa serikali naombeni mtusaidie katika mambo haya, mkawe mabalozi wazuri kulinda amani ya maeneo yetu kwa maslahi ya taifa letu."
Aidha Mhe Chalamila amewataka wamiliki hao kufanya kazi kutokana na leseni zao zinavyowataka huku mchakato wa kurekebisha sheria ya muda inayo wataka kufungua biashara saa 10 jioni mpaka saa 5 usiku kwa siku za kazi na siku za mwisho wa juma kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 6 usiku unaendelea.
"Ni lazima tufanye kazi kwa pamoja ili mkoa wetu uwe wa kibiashara na biashara zifanyike saa 24, kwa kufuata sheria ili pia tuufanye Mkoa huu kuwa wa tofauti na mikoa mingine na sisi kama serikali tutafute namna ya kuwasaidia wafanyabiashara kwasababu Serikali inapata mapato kutoka kwao ambayo husaidia kuboresha huduma mbalimbali za kijamii," alisema RC Chalamila.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa wamiliki wa baa na kumbi za starehe(UBAKUTA), Mponjoli Mwakabana aliiomba serikali kuboresha sheria hiyo kwasababu haindani na wakati huu.
Sambamba na hilo wamiliki hao walipata nafasi ya kueleza kero, maoni na ushauri kwa Mkuu wa Mkoa, miongoni mwa kero hizo ni usumbufu kwenye mfumo wa leseni, NEMC na polisi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa