Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Septemba 15, 2023 amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya magari yaendayo kasi Nyerere Road ambayo inatoka mjini hadi Gongo la Mboto yenye urefu wa kilometa 23.3.
RC Chalamila amesema Barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi wa nchi yetu, vilevile ni ya Kidiplomasia na ni Barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl JK Nyerere. " Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anataka kuona Barabara hiyo inaisha mapema tena hata kabla ya muda uliowekwa kwa mujibu wa mkataba ili kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi" Alisema RC Chalamila
Aidha Mhe Albert Chalamila amemtaka mkandarasi Sino Hydro kuongeza kasi ya ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati pia amemtaka kuzingatia misingi ya mahusiano mazuri na wawekezaji walioko kando ya barabara hiyo kwa kuhakikisha kunakuwa na njia za kuweza kuingia kwenye miradi yao
Mhe RC Chalamila amebainisha Mhe Rais amekuwa akifanya maboresho makubwa ya miundo mbinu katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo dhamira yake ni kuona maboresho ya miundo mbinu yanafungua fursa ya watu kufanya biashara saa 24 na sio saa 12 kama ilivyo sasa ukizingatia Dar es Salaam ni jiji la kibiashara.
Kwa upande wa Mhandisi Frenk Mwingira ambaye ndiye msimamizi wa mradi huo amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kukamilisha kwa wakati Ujenzi wa Barabara hiyo licha ya kuwa mkandarasi yuko nyuma kidogo kutokana na Changamoto mbalimbali lakini maendeleo ya Ujenzi wa Barabara hiyo yanakwenda vizuri
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa