-Aitaka TEMESA kufanya maboresho ya utoaji huduma ili ziwe rafiki kwa wananchi
-Asema wakati ni sasa kushirikisha sekta binafsi katika utoaji wa huduma za kivuko hicho
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 15, 2024 ametembelea na kufanya ukaguzi wa mwenendo wa utoaji huduma katika kivuko cha Feri - Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila wakati akikagua mwenendo wa utendaji kazi na mazingira ya kivuko hicho ameitaka TEMESA kufanya maboresho makubwa ya mazingira ya utoaji huduma ambayo yatakuwa rafiki kwa watu wote wanaotumia huduma hiyo ya kivuko
Aidha RC Chalamila amesema ni vizuri kufungua milango kwa sekta binafsi kuwekeza katika kivuko hicho ili kuwe na huduma Bora ambazo zitavutia wananchi mfano mzuri kwa sasa Kivuko binafsi kimekuwa kimbilio la watu kuliko kivuko cha Serikali tafsiri yake ni kuwa sekta binafsi inaweza kufanya vizuri zaidi.
" Rais hawezi kuwaamulia kila kitu ukipewa dhamana umeaminiwa , hivyo kuwa mbunifu" Alisema Chalamila
Mwisho katika ziara hiyo Mhe Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo na Mhe Halima Bulembo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni wote kwa pamoja wamesema wananchi Ilala na Kigamboni wanataka kupata huduma bora za kivuko na sio vingine hivyo kila mmoja afanye kazi kwa weledi katika eneo lake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa