-Akagua miundombinu ya barabara, maeneo yaliyotuama maji na mabonde ya mito mbalimbali aliyoathiriwa nyakati za mvua.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 28,2024 akiwa na timu ya wataalam amekagua maeneo mbalimbali Katika Mkoa huo ambayo aliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua kwa kutumia ndege maalum ya TANAPA.
RC Chalamila akiongea na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl JK Nyerere Terminal I kabla ya kuruka na ndege hiyo amesema mvua zilizonyesha katika Mkoa huo zimeleta athari kubwa hivyo ameona ni vema kukagua kujionea hali halisi ili badaye kwa pamoja kuja na Suluhu ya athari zilizojitokeza.
Ambapo amesema ameambatana na wataalam wa Ardhi, Kamati ya usalama, mganga Mkuu wa Mkoa, wataalam wa bonde pamoja na Viongozi wa chama cha mapinduzi.
Katika ukaguzi wake RC Chalamila amesema watakagua athari za mvua katika mabonde ya mito mbalimbali ikiwemo Msimbazi, Nyakasangwe, Mpigi na mto Mzinga, vilevile maeneo ambayo yamejengwa holela, pia maeneo ambayo maji yametuama ili yasisababishe magonjwa, na barabara ambazo zilipata athari za mvua ili badaye kuja na namna bora ya kurejesha miundombinu hiyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa