Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, leo Oktoba 11, 2024, ameungana na wakazi wa Mtaa wa Masaki-Kinondoni kujiandikisha katika Kituo cha Ofisi za Serikali za Mitaa katika Mtaa huo.
Katika tukio hilo, Mhe. Chalamila alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka Wilaya zote kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kushiriki katika uchaguzi huo muhimu.
Vilevile Mhe. Chalamila alisisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kuchagua viongozi watakaoweza kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili katika jamii kwakuwa viongozi sahihi ni muhimu katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuhakikisha kwamba maendeleo endelevu yanafikiwa.
Mwisho, Mhe. Albert Chalamila aliahidi kuwa Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na amani pamoja na ulinzi wa kutosha wakati wote wa zoezi hilo hadi wakati wa uchaguzi tarehe Novemba 27, 2024 itakuwa ni siku ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, hivyo zoezi hilo litafanyika kwa uhuru na haki bila ghasia yoyote
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa