Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 20, 2023 amefungua warsha elekezi ya maandalizi ya Dira ya maendeleo ya Taifa itakayotumiwa na Taifa letu kati ya mwaka 2025 hadi 2050.
Warsha hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Anatouglo Mnazimmoja na kuhudhuriwa na Wataalam kutoka Wizara ya fedha, Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakuu wa vyombo vya Usalama, Wakuu wa Taasisi za Umma, Taasisi binafsi, Taasisi za kiraia, Viongozi wa Dini na makundi maalum katika Mkoa huo.
RC Chalamila akifungua warsha hiyo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maandalizi ya machakato wa Dira mpya ya maendeleo ya Taifa kwani ni ukweli usiopingika Taifa lisilo na Dira ni Taifa mfu.
Aidha Mhe Chalamila amesema yako mambo muhimu ya kuzingatia ambayo Serikali imeanisha katika mchakato huo kama: Kuimarisha uchumi uliopo na kulinda mafanikio yaliyopatikana, matumizi ya fursa ambazo hazijatumiwa ipasvyo hadi sasa, Elimu ya Sayansi, Elimu ya ufundi na ufundi stadi, utafiti na Ubunifu ili kukuza ujuzi, kutavutia na kuasili teknolojia ili kukuza tija katika sekta zote za uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuingia ubia wa kimkakati.
Mdau kutoka taasisi binafsi akitoa maoni wakati wa warsha hiyo.
Vilevile kubaini uhalisia wa rasirimali zote, kujifunza kutoka nchi zilizoendelea kwa kasi kuanzia mwaka 1960 hususani bara la Asia na nchi nyingine zilizo jikwamua kutoka katika uchumi wa kati, pia wananchi wote watapata fursa ya kutoa maoni yao katika mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa mpya inayotarajiwa kuleta maguzi makubwa ya kiuchumi na kijamii.
Hata hivyo Mhe RC Chalamila amesema makundi mahususi kama Bunge, mahakama, Sekta binafsi, Idara za Serikali, vyombo vya Usalama, Taasisi za Elimu, Asasi za kiraia, na Watanzania waishio ughaibuni, na washirika wetu wa maendeleo watapatiwa muda wa kutosha kushiriki mchakato huo muhimu pia wizara zote, Taasisi za Umma, wakala, idara zinazojitegemea, Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za mitaa, sekta binafsi, wanadiaspora na wadau wa maendeleo wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu ya maandalizi ya Dira mpya.
Sambamba na hilo Prof Samwel Wangwe amesema kufunguliwa kwa warsha hiyo kunaashiria kuanza uhamasishaji wa ushiriki wa wadau wote katika mchakato wa maandalizi ya Dira mpya ya Taifa ili waweze kutoa maoni ambayo yatafanikisha uandaji wa Dira hiyo kwa maendeleo endelevu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa