-Atoa rai kwa washiriki wote kuwa mabalozi na walimu wazuri kuhusu ulinzi wa miundombinu ya TPDC
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 15, 2024 amefungua semina muhimu kwa viongozi wa Dini na Serikali wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao wamepitiwa na miundombinu ya gesi asilia katika ukumbi wa mikutano wa JNICC, Semina ambayo imeandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
RC Chalamila akifungua Semina hiyo amepongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kufanikisha semina hiyo muhimu kwa Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Dini wa Jijini Dar es salaam ambao wamepitiwa na miundombinu ya gesi asilia kwenye Wilaya za Ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke, ambapo amesema hilo linadhihirisha ushirikiano na uhusiano mzuri wa kidugu, uliopo kati ya TPDC na maeneo yaliyopitiwa na bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.
Aidha RC Chalamila amesema kuwa Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa kielelezo katika bara letu la Afrika na Dunia kiujumla katika mapambano ya kupiga vita matumizi ya nishati chafu ya kupikia, TPDC kupitia gesi asilia ni mdau mkubwa katika kuhakikisha hili
Vilevile amewapongeza Viongozi wote walioshiriki warsha hiyo muhimu ambayo itawajengea uwezo katika kuisemea vyema Serikali kwenye sekta ya mafuta na gesi
Sanjari na hilo RC Chalamila amesema Serikali imeweka mikakati mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wake wanatumia nishati safi ya kupikia ambapo tunategemea kwamba ndani ya miaka 10 kuanzia 2024-2034 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.Hivyo kupitia TPDC naamini Wananchi wengi watanufaika na matumizi ya gesi asilia kwenye magari, majumbani, viwandani na kwenye umeme.
Mwisho Mhe Mkuu wa Mkoa amewatakia wote kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yao, na kufungua rasmi semina hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa