Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 13, 2023 amefungua semina elekezi kwa Mawakala wa Bima zaidi ya 1300 katika Ukumbi wa Mikutano Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.
Akifungua mafunzo hayo RC Chalamila amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua fursa nyingi za uwekezaji, mataifa mbalimbali yanakuja kuwekeza hivyo Taasisi za bima, na Mawakala ni wakati muafaka wa kuitumia fursa hiyo kikamilifu kwa kuwa Rais amewaongezea wadau wa Bima " Muhimu zaidi kwa makampuni ya bima ni kuzingatia misingi ya Uaminifu na Uadilifu pale majanga yanapotokea mchakato ufanyike kwa wakati" alisema RC Chalamila
Aidha RC Chalamila amewataka mawakala wa bima kujiuliza maswali yafuatayo kwa nini tuko hapa? Mteja wako ni nani? ambapo kupitia maswali hayo juhudi kubwa iwekwezwe katika kuelimisha na kuhamasisha jamii umuhimu wa kuwa bima za aina mbalimbali ambazo zitawanusuru wanapofikwa na majanga " tufikie pahala bima iwe ni utamaduni katika jamii zetu kama ilivyo kula chakula unvyohisi njaa." Alisisitiza Chalamila
Kwa Upande wa Mwakilishi wa Kamishana wa Bima Ndg Frank Shangani amesema mafunzo hayo yamehusisha makampuni ya Bima zaidi ya 1300 ambapo lengo kubwa ni kuelimishana na kukumbushana namna ya kuendeleza sekta hiyo kwa masilahi mapana ya Wananchi na amemuhakikishia mkuu Mkoa kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo yake
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa