Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Novemba 28, 2023 amefungua Mkutano wa wadau wa Benki ya Maendeleo (TIB) katika ukumbi wa mikutano JNICC - Dar es Salaam
RC Chalamila amepongeza Bodi na menejimenti ya Benki ya maendeleo TIB kupitia mafanikio yaliyopatikana toka kuanzishwa kwake mwaka 1970.
Aidha RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya uwekezaji katika Benki hiyo kwa kuwa TIB ina mkono wa Serikali ni ukweli usiopingika Rais asingekuwa na mapenzi na Benki hiyo isingekuwepo hadi " kuendelea kukua kwa Benki hiyo kunatanua fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania ambao wajipatia kipato na kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa" Alisema RC Chalamila
Kwa upande wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Lilian Mbassy amesema lengo la mkutano huo unaohusisha wadau wa Benki hiyo pamoja na Watumishi ni kutoa nafasi ya pamoja kujadili fursa zinazopatikana katika Benki ya TIB ili wadau waweze kuzitumia fursa hizi kwa masilahi mapana.
Vilevile amesema Benki hiyo inatoa mitaji/ mikopo ya muda mrefu, ya kati na kwa ajili ya maendeleo ya viwanda na uwekezaji katika sekta mbalimbali hapa nchini
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa