-Awataka kuyazingatia mafunzo hayo kwa kuyafanyia kazi ili kuleta mabadiliko chanya katika biashara na maisha yao
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 26, 2023 amefungua mafunzo ya wanawake Wajasiria mali kutoka katika mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa JKT Mgulani Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Akifungua mafunzo hayo ambayo yanaendeshwa kwa udhamini wa Mfuko wa fursa sawa kwa wote (Equal Opportunities For all Trust Fund) RC Chalamila amemshukuru Mama Anna Mkapa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kumwezesha mwanamke kiuchumi ambapo ameweza kuandaa mafunzo ambayo yanajenga thamani ya mwanamke katika kukuza uchumi wa Taifa vilevile kuboresha malezi ya familia.
Aidha RC Chalamila amewataka wanawake Wajasiria mali hao mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo wakirudi katika mikoa yao kufanyia kazi mafunzo hayo ili kuweza kuboresha biashara zao na maisha yao
Kwa upande wa Mama Anna Mkapa akitoa taarifa ya mafunzo hayo yenye kauli mbiu " Ukuzaji na Ubunifu ni Msingi wa Biashara Endelevu " licha ya kufundisha mada ya ujasiriamali pia watapatiwa mafunzo ya Afya ya familia na namna ya kujikinga na maradhi hatarishi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa