-Asema utekelezaji wa miradi ya TANESCO uko kwenye ngazi ya mitaa ambayo huongozwa na wenyeviti wa Serikali za Mitaa
-Aipongeza TANESCO kwa kuandaa kikao na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Ubungo kwa kuwa ni wadau muhimu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Altbert Chalamila leo Juni 24, 2025 amefungua kikao kazi kilichoandaliwa na TANESCO kwa ajili ya Wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
RC Chalamila akifungua kikao kazi hicho amesema wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali kwa kuwa miradi hutekelezwa katika maeneo yao ya kiutawala hata miradi mingi ya TANESCO iko kwenye mitaa hivyo "ni imani yangu kuwa kupitia kikao kazi hiki wenyeviti wote wanakwenda kuwa mabalozi wa kueleza huduma nzuri zinazotolewa na TANESCO pia kulinda miundombinu ya Shirika hilo" Alisema RC Chalamila.
Aidha ameipongeza TANESCO kwa kuona umuhimu wa kukutana na kundi hilo muhimu ili liweze kufahamu kwa kina majukumu ya shirika hilo lakini pia kutoa mawazo na ushauri wa namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma za nishati ya umeme kwa wananchi hususani katika mitaa yao.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bwana Lazaro Twange amesema Shirika hilo kwa kutambua Wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu likaona liandae kikao kazi kwa ajili yao ili kutengeneza mfumo mzuri wa mawasiliano ambao utatusaidia kujua wananchi wanasemaje kuhusu huduma za TANESCO pia wenyeviti wawe na uwezo wa kuelewa nini kinafanywa na shirika pamoja na kuwaelimisha wananchi walioko katika maeneo yao.
Mwisho Mkurugenzi wa TANESCO Bwana Lazaro Twange amemkabidhi RC Chalamila na Viongozi wachache wa Mitaa Jiko la Umeme ambalo linatumia umeme kidogo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya Nishati safi kwa Jamii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa