RC CHALAMILA AFANYA KIKAO NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI PAMOJA NA VIONGOZI WA NACONGO-DSM
-Atoa elimu na umuhimu wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika Mkoa.
-Ahamasisha uimarishwaji wa ushirikiano Kati ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 22, 2024 amekutana na kufanya kikao na viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika ukumbi wa Karimjee-Posta ikiwa ni katika Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya serikali Mkoa wa Dar es salaam.
RC Chalamila kupitia kikao hicho alipata wasaa wa kutoa elimu na kuelezea namna bora ya kuendendesha Mashirika yasiyo ya kiserikali na kufahamu zaidi majukumu yake kwa kupeana ushirikiano madhubuti na kujua namna ya kuhimili na kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika kukuza maendeleo ya jamii kupitia kaulimbiu yao inayosema "Mashirika yasiyo ya kiserikali yashirikishwe katika Utawala Bora"
Vilevile RC Chalamila amehimiza NGOs kuoanisha mipango yao na vipaumbele vya serikali,hususani katika maeneo ya kupunguza umaskini,usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa vijana na hata kushiriki kwenye mijadala ya dira ili kujua fursa mbalimbali zipatikanazo katika dira hizo.
Aidha Mhe. Chalamila ametoa maagizo kwa viongozi hao ikiwemo kulinda desturi,kuwasilisha fedha za utekelezaji,kuhakikisha wanufaika wanashiriki ipasavyo ili kuwezesha uendelevu wa miradi. Ameongeza kwa kusema kuwa mashirika haya yanapaswa kuwa endelevu na kushirikiana na serikali kwa maendeleo ya Taifa zima
Sanjari na hayo, Mwenyekiti wa bodi ya Mashirika yasiyo ya kiserikali Bi. Mwantumu amewahakikishia viongozi hao kupata matokeo mazuri kutokana na vikao mbalimbali vinavyowekwa kutokana na ushirikiano aliouonesha Mhe. Chalamila katika kikao hiki Cha Leo na katika vikao vingine pia ametumia fursa hiyo kuwasihi vijana kupambanua uzalendo wao na kutohamasisha kufanya mambo mabaya kwa jamii na kuelekezana mambo yalio Bora kwa kuwa Taifa hutegemea sana vijana kwa jamii ya baadae
Mwisho RC Chalamila ameshukuru viongozi na wadau wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ushirikiano na kazi wanazotekeleza na kuwahamasisha kufanya kazi kwa weledi na kupanua wigo wa ushiriki katika jamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa