-Akagua uwekezaji mkubwa wa viwanda vya Kisasa katika eneo hilo.
-Afurahishwa na ajira za watu zaidi ya 4500 katika kiwanda hicho.
-Aagiza wataalam wa Ardhi na Mipango miji katika wilaya zote za Mkoa kutenga na kupima meeneo zaidi ya uwekezaji.
-Azitaka Taasisi ambata kuwezesha wawekezaji walioko katika eneo hilo kwa mfano DAWASA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila Leo Septemba 10,2024 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua uwekezaji eneo la EPZA (Export Processing Zone Authority) iliyopo Ubungo-External.
Akiwa katika eneo hilo RC Chalamila alipata taarifa fupi ya uwekezaji wa aina mbalimbali ndani ya EPZA na kukagua uzalishaji wa bidhaa za nguo katika moja ya viwanda vilivyomo katika eneo hilo.
Pia, Mheshimiwa Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake makini ambao umewezesha uwekezaji wa zaidi ya Dollar Milioni 2 katika kituo hicho.
Aidha Mhe. Chalamila ameagiza wataalam wa Ardhi na Mipango Miji kutenga na kupima maeneo zaidi ya uwekezaji yenye miundombinu rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje.
Sanjari na hilo RC Chalamila amefurahishwa na fursa nyingi za ajira kwa wazawa ambapo amesema zaidi ya watu 4500 wamepata ajira kutokana na uwekezaji huo.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa EPZA Bw. Charles Itembe amesema sekta hii imewezesha ajira kwa vijana wengi wa kitanzania pia usahili wa kampuni takribani 80 ambazo zinachagiza ongezeko la uwekezaji na uzalishaji.
Mwisho, RC Chalamila amehakikishia watanzania hususani wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam kuwa Tanzania ni salama sana, Jeshi la Polisi linaendelea kudhibiti vitendo vidogovidogo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa