Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ametoa maagizo hayo leo Desemba 22, 2023 wakati wa ziara yake ya kukagua machinjio hayo yanayojengwa kwa thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 19 ambapo hadi sasa yamekamilika kwa asiliamia 97.
RC Chalamila alisema machinjio hayo yaliyoanza kujengwa tangu 2019 ni ya kisasa yenye uwezo wa kuchinja ngo'mbe elfu moja kwa siku na ikiwa ng'ombe mmoja akachinjwa kwa sh 20,000 serikali itapata mapato yatakayosaidia kuendesha gharama za uendeshaji ambazo ni kubwa kutokana na mitambo yote inayotumika inatumia umeme tu.
Pia RC Chalamila alikemea vitendo vya rushwa kwa watumishi vilivyobainishwa na wafanyabiashara hao hivyo aliagiza kamati iundwe itakayochunguza mwenendo na uadilifu wa watumishi.
"Na baada ya kukamilika kwa kamati hiyo ndogo ambayo itakuwa na watu mbalimbali, wakiwemo watu wa usalama, watu wa TAKUKURU, watu wa utumishi wa umma, wahandisi na wengine itatupatia majawabu ya miundombinu ya namna ya uchinjaji na mchakato wote," alisema RC Chalamila.
Aliendelea, "Nitoe rai kwa watu wanaohusika na ujenzi huu hasa kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wahakikishe wanakamilisha ujenzi huo na kufunga vifao vyao haraka iwezekanavyo ili Rais Samia Suluhu Hassan atakavyotembelea hapa kwa ajili ya kuzindua au kufanya mengine kusiwe kuna dosari ya aina yoyote."
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo alitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa kwa kufanya ziara na kuahidi yote waliyoagizwa wataenda kuyafanyia kazi zikiwemo changamoto zilizosababisha mradi huo kutokukamilika kwa wakati.
Awali mwenyekiti wa wafanyabiashara machinjioni hapo, Emanuel Siliake alimueleza RC kuwa kuna baadhi ya watumishi wamekuwa na utendaji mbaya, vitendo vya rushwa na kuchukua nyama zao kwa kutumia nguvu na kutusababishia wao kupata hasara.
Pia RC Chalamila alifika katika viwanja vya msikate tamaa vilivyopo kata ya Vingunguti na kushiriki zoezi la utoaji wa vitambulisho vya NIDA kwa wananchi, na aliwasihi wananchi wakachuke vitambulisho vyao kwakuwa baada ya mwezi mmoja kupita wataenda kuvichukua kwa pesa kama gharama yakuhifadhiwa kwa mkoa wa DSM, Sambamba na hilo aliwaambia wananchi washerehekee sikukuu kwa amani sababu ulinzi upo Mkoa umejipanga vizuri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa