-Mamia ya Wananchi wa Jimbo la Ukonga wafurika kutoa kero zao
-Akemea vikali tabia za baadhi ya viongozi kujipatia fedha kwa kuwatapeli watu wa kipato cha chini
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 28,2024 akiwa katika Mkutano wa hadhara Jimbo la Ukonga Wilaya ya Ilala amesikiliza kero za mamia ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Pugu Stesheni hadi giza limeingia bado akaendelea kuwasikiliza wananchi hao.
RC Chalamila akiwa katika muendelezo wa zaira zake alianza kwa kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo la Ukonga ikiwemo mradi wa barabara ya Kitunda-Msongola ambayo iko katika hatua ya kujengwa kwa kiwango cha lami ya zege, Hospitali ya Wilaya Kivule, na Ujenzi wa mradi wa tanki kubwa la maji Bangulo Pugu Stesheni ambapo amesema miradi yote hiyo inatekelezwa kutokana na uwekezaji mkubwa wa fedha nyingi unaofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha RC Chalamila baada ya kupitia miradi hiyo alipata wasaa wa kuongea na wananchi ambapo amekemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi katika ngazi za mitaa na Kata, ambavyo husababisha migogoro mingi tena kwa bahati mbaya wananchi wa kipato cha chini ndiyo waathirika wakubwa.
Sanjari na hilo RC Chalamila amewahakikishia wananchi wa jimbo la Ukonga kutofumbia macho migogoro isiyo yalazima dhamira yake ni kuona jamii yenye ustawi.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amemshukuru mkuu wa Mkoa kwa kutenga muda wake kufanya ziara katika wilaya hiyo ambapo ameahidi kufanyia kazi maagizo yake yote kwa masilahi mapana ya wanaukonga na Ilala kwa ujumla
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa