-Asema elimu iendelee kutolewa kwa jamii kuhusu vitendo vya ukatili
-Aagiza kila kikao kikiketi kitoke na madhimio ya kupambana na vitendo vya ukatili
-Aelekeza kutengwa kwa bajeti katika Halmashauri zote kwa ajili ya mapambano ya vitendo vya ukatili
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila leo Julai 19,2024 ameongoza kikao cha kamati ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa Mkoa huo kilichokuwa kinafanyika katika ukumbi wa Afya ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Boma.
Akiongea na wajumbe wa kamati hiyo Dkt Toba amesema bado vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinadhidi kukithiri katika jamii tumekuwa tukishuhudia mara kwa mara vitendo hivyo ambavyo saa nyingine vinachangiwa na imani za kishirikina hivyo ni muhimu sana kamati ya MTAKUWWA kuendelea kutoa elimu kwa jamii dhidi ya vitendo hivyo ili ifike hatua ya kuvikomesha kabisa.
Aidha ameagiza kila kikao cha kamati kinavyoketi kihakikishe kinatoka na maadhimio mahususi ya kutokomeza vitendo vya ukatili katika Mkoa huu,kila mjumbe apitie majukumu yake, na kuyajua ili vikao vinapofanyika wajumbe wawasilishe namna walivyotekeleza majukumu yao kwa masilahi mapana ya jamii.
Vilevile Dkt Toba amesema viko vitendo vingi vya kikatili vinafanyika katika fukwe pia kwa kina mama wanao omba mitaani wakiwa wamebeba watoto wadogo, ni wakati muafaka wa kufuatilia kwa karibu ili kuja na suluhu ya matendo hayo ya kikatili.
Sanjari na hilo Katibu Tawala wa Mkoa ameagiza Halmashauri zote tano za Mkoa kutenga bajeti ambayo itatumika kwenya mapambano dhidi ya ukatili ambao umekuwa tishio katika jamii zetu
Mwisho Dkt Toba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wajumbe wa kamati lakini pia idara mbalimbali ambazo zinahusika moja kwa moja ikiwemo Ustawi wa Jamii ,Maendeleo ya Jamii na Elimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa