Katibu tawala wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaan Ndg Hashimu Rugwa akiongea wakati wa hafla hiyo Mnazimmoja Ilala Dar es Salaam.
# Asema mchango wao utaendelea kuenziwa milele
# Akiri kupokea ujumbe wao na kuufanyia kazi
# Awaasa kupata Chanjo ya Uviko 19
# Awataka Wakurugenzi wote kusimamia Uundwaji wa Mabalaza ya Wazee Katika Mitaa yote
# Mwenyekiti wa Balaza la Wazee Dsm apongeza kushirikishwa
# RMO asema Wazee wataendelea kutunzwa, kuheshimiwa na kulindwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Hassan Rugwa Leo tarehe 01 Oktoba, 2021 ameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
Akiwa katika Maadhimisho hayo Bw. Rugwa amesema mchango wa Wazee kwa taifa hili utaendelea kuenziwa milele na hii tunaiona toka enzi za Utawala wa Awamu ya Kwanza mpaka sasa ambapo Rais Samia alipoapishwa tu alikutana na Wazee ili apate maoni yao
Hata hivyo Katibu Tawala amekiri kupokea ujumbe wao uliosomwa na Katibu wa Balaza la Wazee Bw. Frenki Macha na kusema kuwa yote waliyoyasema yakiwemo Kupatiwa Ofisi, kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa, Usafiri, na Huduma ya Matibabu yatayafanyiwa kazi
Vile vile amewaasa Wazee hao kuitumia siku Yao vema kwa kupata Chanjo ya Uviko 19 kwani ugonjwa huo upo na unaua aidha walio hatarishi zaidi ni Wazee hivyo ni vema wakachanjwa ili waweze kuwa salama
Wakati huo huo Katibu Tawala Bw. Rugwa amewataka Wakurugenzi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia Uundwaji wa Mabalaza ya Wazee Katika Mitaa yote
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Balaza la Wazee wa Dar es Salaam Bw.Ramadhani Matimbwa amepongeza juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Maadhimisho ya Siku hiyo na kuwashirikisha Wazee hao kikamilifu
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashidi Mfaume amesema kuwa mchango wa Wazee ni Mkubwa kwa Taifa hili hivyo wataendelea kuenziwa, kutunzwa na kuheshimiwa na ndio maana Kauli mbiu ya mwaka huu inawataka washirikishwe katika fursa mbalimbali bila kujali uzee wao.
"Serikali imeendelea kuwapatia Wazee huduma mbalimbali ikiwemo Matibu kwa Afya zao". Alisisitiza Dkt. Rashidi
"MATUMIZI SAHIHI YA KIDIGITALI KWA USTAWI WA RIKA ZOTE".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa