- Ataja ratiba ya Mwenge kukimbizwa Dar es Salaam
-Asisitiza Umuhimu wa Mwenge huu, Kauli Mbiu na Ujumbe wake
- Ataja thamani ya Miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru
-Akabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni ambapo DC huyo akiri kuupokea na kuukimbiza katika Wilaya yake
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Hassan Rugwa amepokea Mwenge wa Uhuru Leo tarehe 10 Aprili 2022 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Bunju "A" ukitokea Mkoa wa Pwani
Baada ya kuupokea Mwenge huo wa Uhuru Ndg. Hassan Rugwa ametaja ratiba ya ukimbizwaji wa Mwenge katika Mkoa wa Dar es Salaam kuwa tarehe 10/05/2022 Utakimbizwa Kinondoni, tarehe 11/05/2022 Utakimbizwa Ubungo, tarehe 12/05/2022 Ilala, tarehe 13/05/2022 Kigamboni na kumalizika Temeke tarehe 14/05/2022 ambapo tarehe 15/05/2022 utakabidhiwa Mkoa wa Kusini Pemba
Aidha Katibu Tawala amesisitiza Umuhimu wa Mwenge wa Uhuru wa 2022 unaosisitiza Sensa ya Watu na Makazi chini ya Kauli Mbiu " Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo; Shiriki Kuhesabiwa tuyafikie Maendeleo ya Taifa" na Ujumbe wa Kudumu wa Mbio za Mwenge kuhusu Mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe na Rushwa
Ndg. Hassan Rugwa amesema jumla ya Miradi 28 yenye thamani ya *Shilingi Bilioni 16. 4 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru ambapo Miradi hiyo ipo iliyokamilika na iliyopo katika hatua mbalimbali za utekelezaji
Hata hivyo Katibu Tawala ameukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe ambaye amekiri kuupokea na kuukimbiza katika Wilaya yake ya Kinondoni
MWENGE OYEEEEEE
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa