-Aelezea malengo mahususi ya Sera ya vihatarishi
-Ainisha majukumu ya Katibu Tawala Mkoa, Mratibu wa Usimamizi wa Vihatarishi, Wakuu wa Sehemu na Vitengo, Mabingwa wa Vihatarishi, Ukaguzi wa Ndani na Wafanyakazi wote
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba A. Nguvila amefungua mafunzo ya Risk Champions Mkoa wa Dar es Salaam Leo tarehe 23 Mei, 2024 katika Ukumbi wa DMDP- Ilala kwa kusema Usimamizi wa Vihatarishi unahusiana na Utamaduni, Taratibu na Miundo inayoelekezwa kwenye usimamizi madhubuti wa fursa zinazowezekana na athari za mazingira ya kiutendaji katika Sekretarieti ya Mkoa wa Dar es Salaam
Dkt. Nguvila ameelezea malengo mahususi ya Sera ya Usimamizi wa Vihatarishi kuwa ni:- -Kuwasilisha dhamira ya Sekretarieti katika usimamizi wa Vihatarishi na kusaidia katika kufikia malengo yake kimkakati na kiutendaji, -kurasimisha na kuwasilisha mbinu thabiti ya Kudhibiti hatari kwa Shughuli zote za Sekretarieti na kuanzisha utaratibu Mzuri wa utoaji wa taarifa, -Kuhakikisha kwamba hatari zote kubwa za Sekretarieti zinatambuliwa, kutathminiwa, kudhibitiwa na kutolewa taarifa, -kuweka uwajibikaji kwa wafanyakazi wote kwa ajili ya Usimamizi wa hatari katika maeneo yao na kuwataka watumishi wote watambue ya kwamba usimamizi wa Vihatarishi ni jukumu lao la msingi kiutendaji
RAS Nguvila ameainisha majukumu ya *Katibu Tawala wa Mkoa* kuwa ni pamoja na kuweka Taratibu zinazofaa ili kusimamia utekelezaji wa Usimamizi madhubuti wa Sera ya vihatarishi, kubuni, kutekeleza na kuimarisha mfumo wa Usimamizi wa vihatarishi. *Mratibu wa Usimamizi wa Vihatarishi* anafanyakazi ya kumsaidia Afisa Masuuli hivyo wajibu wa kuratibu Juhudi katika kubuni mfumo wa Usimamizi wa Vihatarishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kwa Shughuli za kila siku zinazohusiana na kuratibu, kudumisha na kufanya mfumo uweze kufanya kazi ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam *Wakuu wa Sehemu na Vitengo*(Wamiliki wa Vihatarishi) Kudhibiti Vihatarishi katika maeneo yao, kupitia orodha na kuhuisha taarifa ya vihatarishi Mara kwa Mara na utayarishaji wa taarifa za robo mwaka za utekelezaji za utekelezaji wa udhibiti wa hatari *Mabingwa wa Hatari*(Risk Champions) Hawa hufanyakazi ya Kudhibiti Vihatarishi katika Sekretarieti sambamba, kuandaa na kuhuisha rejista ya vihatarishi vya Idara na kufanya mapitio ya Mara kwa Mara kwa Vihatarishi katika miradi ya maendeleo *Ukaguzi wa Ndani* kutathmini ufanisi wa Shughuli za usimamizi wa Vihatarishi katika kuhakikisha kwamba hatari kuu zinazoikabii Sekretarieti zinadhibitiwa ipasavyo na kuzingatia kazi ya Ukaguzi wa Ndani juu ya hatari kubwa Kama inavyotambuliwa na usimamizi *Wafanyakazi wote* watakuwa na jukumu la kutambua hatari na kutoa taarifa ya vihatarishi kwa sehemu na Kitengo kinachohusika. Inapowezekana wanapasw pia Kudhibiti hatari hizi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa