-Akuta huduma nzuri inatolewa hospitalini hapo
-Abaini wingi wa wagonjwa hospitalini hapo na uchache wa watumishi na kumuagiza Mkurugenzi na DMO kuongeza watumishi
-Aagiza RMO, DMO's kutembelea Hospitalini ,Vituo vyao Afya na Zahati usiku na mchana kukagua huduma zinazotolewa huko
-Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mohamedi Mang'una akiri kupokea maelekezo na kuahidi kuyasimamia ipasavyo
-Baadhi ya ndugu za wagonjwa waliokuwepo hapo wasema huduma hapo ni nzuri
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba A. Nguvila akiambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mohamedi Mang'una amefanya ziara ya kushtukiza ya usiku wa manane tarehe 06 Septemba, 2024 katika Hospitali ya Wilaya ya Mbagala Rangi tatu na kukuta huduma nzuri inatolewa katika Hospitali hiyo
Dkt. Nguvila amebaini uwepo wa wagonjwa wengi wanaofika kuhudumiwa katika Hospitali hiyo na uchache wa watumishi wanaotoa huduma na kumuagiza hapo hapo Mkurugenzi wa Temeke kupitia Idara ya Afya kuhakikisha wanaongeza watumishi katika Hospitali hiyo ili kupunguza msongamano wa wagonjwa sambamba na kupata huduma Bora kwa wakati
Hata hivyo RAS Nguvila amemuagiza RMO, DMO's kutembelea katika Vituo mbalimbali vya Afya usiku na mchana ili kujionea huduma zinazotolewa huko na kuyafanyia kazi mara Moja mapungufu pindi wanapokutana nayo
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mohamedi Mang'una amekiri kupokea maagizo yote yaliyotolewa na Katibu Tawala wa Mkoa na kuahidi kuyasimamia ipasavyo ili wananchi wa Temeke waendelee kupata huduma Bora za Afya, aidha amewaasa wananchi wasisite kutoa taarifa kupitia mawasiliano yaliyopo pindi wanapopatwa na kadhia yoyote ili kadhia zao zipatiwe ufumbuzi wa haraka
Wakati huo huo baadhi ya ndugu wa wagonjwa waliokuwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali hiyo wamepongeza huduma zinazotolewa katika Hospitali hiyo na kusema kuwa ni nzuri sana
#Chini ya Uongozi wa SSH tutoe huduma nzuri za Afya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa