- Akemea tabia ya baadhi ya watumishi wa afya wenye lugha Zisizoridhisha kwa Wananchi.
- Atoa Wito kwa Wazazi kuwapeleka watoto kupata chanjo ya Surua kuanzia February 01 hadi February 05.
- Mganga Mkuu DSM Ataka Maandalizi ya Utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
Viongozi na wasimamizi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Dar es salaam Leo wamekutana kwenye kikao kazi Cha kuweka mikakati madhubuti ya maboresho ya utoaji wa huduma Bora za Afya na Maandalizi ya Utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote pindi muswada utakapopitishwa.
Akifungu Kikao hicho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Rehema Madenge ametoa wito kwa watumishi wa afya kuhakikisha wanatoa huduma Bora na zenye ufanisi kwa Wananchi Ili kuondosha Hali ya malalamiko.
Aidha Bi. Madenge Amekemea tabia ya baadhi ya watumishi wa afya wenye lugha Zisizoridhisha kwa Wananchi wanaokwenda kupata huduma huku akipongeza watoa huduma za Afya Mkoani humo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.
Katika hatua nyingine RAS. Madenge ametoa wito kwa Wazazi ambao watoto wao hawakupata chanjo ya Surua kuwapeleka kupata chanjo hiyo inayotaraji kutolewa February 01 hadi February 05 mwaka huu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dr. Rashid Mfaume amewaelekeza Waganga wafawidhi wa Vituo vya Afya kuanza Maandalizi ya kupokea na kutekeleza Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote pindi muswada utakapopitishwa kwa kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa zenye ubora.
Pamoja na hayo Dr. Mfaume amesema takwimu zinaonyesha kati ya *Wananchi 100 ni Wananchi 15 pekee ndio wenye bima ya Afya jambo ambalo linawalazimu kuendelea kutoa Elimu ya umuhimu wa Bima ya Afya.
Kikao hicho kilichojumiisha waganga wakuu wa Wilaya, Makatibu wa Afya na Waganga wafawidhi kutoka Vituo 142 vya Afya Mkoani humo kimetoa fursa pia ya kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa