Katibu Tawala wa Mkoa Bi Rehema Madenge Akiongea wakati wa mafunzo hayo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Rehema Madenge leo Julai 27, 2023 amefungua mafunzo ya kimkakati kwa Kamati ya kudhibiti UKIMWI ngazi ya Mkoa.
Akiongea wakati wa mafunzo hayo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikitekeleza afua za mwitikio wa kitaifa dhidi ya VVU na UKIMWI kwa zaidi ya miongo mitatu (3) tangu kugundulika kwa ugonjwa huo.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa makini wakati wa mafunzo hayo.
Hata hivyo miongoni mwa majukumu ya msingi yanayo tekelezwa ni pamoja kuandaa mpango mkakati wa afua za VVU na UKIMWI pia kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa afua hiyo.
Kwa dhana hiyo Sekretarieti ya Mkoa inajukumu la kuratibu utekelezaji wa masuala ya UKIMWI katika mamlaka za Serikali za Mitaa vilevile Sekretarieti zimetakiwa kuwa na timu au Kamati za kudhibiti UKIMWI (Regional AIDS Team) ambayo ndio hii kupitia wote tuliojumuika hapa
Aidha Bi Rehema Madenge amesema lengo la kamati hii ni kuimarisha uratibu na usimamizi wa afua za VVU na UKIMWI katika Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili zifanye kazi zake za uratibu na usimamizi kwa ufanisi, hivyo kila aliyoko kwenye kamati hii anajukumu kubwa la kufanya kwa mstakabali wa ustawi wa jamii.
Sambamba na hilo mafunzo hayo yameweza kuainisha hali ya VVU na UKIMWI katika Mkoa, wajumbe wamepitishwa kujua mwongozo wa kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza mahala pa kazi, mfumo wa uratibu, mwongozo wa kuziwezesha Sekretarieti za Mikoa kuratibu utekelezaji wa masuala ya UKIMWI katika mamlaka za Serikali za mitaa na Maazimio ya hatua zinazofuata.
Mwisho wajumbe walipata wasaa wa kutoa maoni na michango yao kwa lengo la kufikia dhamira ya Serikali ya kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu yasiyoambukiza mahala pa kazi
Baadhi ya matukio katika picha wakati wa mafunzo hayo mapema leo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa