Washiriki katika kikao cha kupitia Mfumo wa Usimamizi na Uendeshaji wa Bodaboda katika Ukumbi wa DMDP Ilala Jijini Dar es Salaam Mapema leo
- Asema Sekta ya usafiri kwa njia ya Pikipiki au Bodaboda inakua kwa kasi kuwepo kwa mfumo itasaidia Sekta hiyo kutekeleza majukumu yake Kidigitali
-Vilevile mfumo huo Utasaidia kuongeza mapato, pamoja na Ulinzi na Usalama
- Awapongeza UCC (University of Dar es Salaam Computing Center) kwa kubuni mfumo huo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Hassan Rugwa leo Januari 18,2022 amefungua kikao Kazi cha kupitia mfumo wa Usimamizi na Uendeshaji Bodaboda katika Ukumbi wa Mikutano DMDP TARURA Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala amesema sekta hii imekuwa ikikua kwa kasi bila kuwa na mfumo dhabiti inaweza kuwa zahama kwa wananchi badala ya fursa hivyo nawapongeza UCC kwa kuja na mfumo huu.
Aidha Ndg Rugwa amebainisha mfumo utakwenda kurahisisha utendaji kazi wa Serikali ikiwemo Ukusanyaji wa mapato pia Suala la Ulinzi na Usalama kwa mmiliki wa chombo hadi Mtumiaji ambaye ni mwananchi
RAS Rugwa kwa kutambua Umuhimu wa mfumo huo amewataka washiriki kupitia kwa makini ili kuwa na uelewa, kama kuna maoni au mapendekezo wasisite kutoa.
Kikao hicho cha mfumo wa Usimamizi na Uendeshaji Bodaboda DSM kilihudhuliwa na Sekretarieti ya Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Tanroad, Maafisa Biashara, Traffic Police, Wataalam kutoka UCC na Wawakilishi wa Viongozi wa Bodaboda DSM
Kwa upande wa washiriki wa kikao wamepongeza mfumo huo kwa kuwa una tija kwa mmiliki, Mwendesha Bodaboda, Serikali na mwananchi ambaye ni mtumiaji
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa