Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Aboubakar Kunenga amesisitiza Umoja na Mshikamano kwa wafanyakazi wa Mkoa huo na kuwa ndio nguzo pekee ya kufikia malengo husika.
Ameyasema hayo baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kupokelewa na kupata nafasi ya kuongea na wafanyakazi wa Ofisi hiyo.
Amesema tunapaswa kuamini katika Utendaji, kufanya kazi kwa bidii kuwa na umakini wa hali ya juu katika uendaji wa shughuli za kila siku, kuwa na nidhamu, na kujua majukumu yetu ipasavyo.
Awali katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi. Theresia Mmbando alimkaribisha Katibu Tawala huyo katika Mkoa huo na kupata nafasi ya kumtambulisha kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo.
Aidha, alipata nafasi ya kumkabidhi taarifa mbalimbali zitakazosaidia katika kumuongoza Katibu Tawala huyo katika Utendaji kazi wake.
Ikumbukwe kuwa tarehe 28 Julai 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli alifanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa Mikoa,Wizara na Wilaya ambapo Bw. Aboubakar Kunenga aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam na Bi. Theresia Mmbando kuhamishiwa katika Mkoa wa Pwani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa