# Asisitiza Waratibiwe sio kurudi Kiholela
# Asema Watajenga Wenyewe kwa Ghalama zao
#Wafanyabiashara( Wamachinga) watakiwa kutoa Ushirikiano kwa DC, MD na Wataalamu husika
#Wafanyabiashara ( Wamachinga) Wamshukuru Rais Samia, RC. Makalla na DC
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Wafanyabiashara( wamachinga) wa Soko la Karume (Mchikichini) kurudishwa Mara moja katika eneo lao la Biashara soko la Karume
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Amos Makalla leo tarehe 24 Januari 2022 katika Mkutano wake na wafanyabaishara (Wamachinga ) uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Karume ( TFF)
Mhe. Makalla amesema kuwa Rais Samia amesisitiza Wafanyabiashara hao (Wamachinga) waratibiwe vema na uongozi husika na sio kurudi Kiholela
Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema Rais ameelekeza kuwa Wafanyabiashara hao (Wamachinga) Watajenga Wenyewe kwa Ghalama zao lakini wataelekezwa vema (wataratibiwa) na Wataalamu ambapo itapatikana njia ya kuingia na kutoka
Mhe. Makalla ameongeza kuwa Wafanyabiashara hao (Wamachinga) wametakiwa kutoa Ushirikiano kwa Mkuu wa Wilaya Ilala, Mkurugenzi, Wataalamu na Kamati husika
Kwa upande wa Wafanyabiashara (Wamachinga) Wamemshukuru *Rais Samia Suluhu Hassan* *Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam* na *Mkuu wa Wilaya ya Ilala* na *Uongozi wake* kwa kuwarejesha katika maeneo yao ya Biashara na kuahidi kutoa Ushirikiano katika Serikali mwanzo mwisho
Ikumbukwe kuwa Leo tarehe 24 Januari 2022 *Mhe. Makalla* amepokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi ya Uunguaji wa Soko hilo la Karume ambapo Kamati imebaini kuwa Chanzo Cha moto huo ni kutokana na *Mshumaa* ambao uliwashwa na kijana anayesadikika kutumia madawa ya kulevya kisha akasinzia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa