Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe. Albert Chalamila amesema hayo leo Novemba 4, 2023 wakati wa mkutano maalum wa uwasilishaji wa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Uongozi Mahiri wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Yombo (wa chuo kiku cha Dar es salaam)
RC Chalamila alisema chini ya uongozi mahiri wa raisi Dkt Samia Suluhu Hassan wananchi wengi wamesikika na wamefikiwa kwa kuboreshewa na kutatuliwa kero na matatizo yao yaliyokuwa yanawasumbua ikiwemo maji, barabara, umeme, afya, usafiri wa mwendo kasi n.k
Aidha Mhe Chalamil aligusia suala la mshikamano, ushirikiano na amani ambayo ni tunu na rasilimali kwa maendeleo ya nchi wa uwepo wa vyombo vya dola imara ambapo kati ya asilia Mia moja basi asiliamia 95 vyombo hivyo vinafanya kazi nzuri iliyopelekea mpakaTanzania kuwa wenyeji wa mikutano mikubwa ya kimataifa.
Vilevile RC aligusia sekta nyingine mbalimbali zilivyoboreshwa ikiwemo elimu kwa kufuta ada ya kidato cha tano na sita, kuboresha miundo mbinu ya shule kwa kujenga madarasa na nyumba za walimu, mikopo kwa elimu ya juu imeongezeka mpaka elf 10 kwa siku na kuongezeka kwa idadi ya wanufaika.
Pia RC Chalamila alimpongeza Mhe Raisi Dkt Samia maendeleo ya usafiri wa anga kwa kuboresha viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege kubwa yenye kubeba watu 180 na ndege nyingine ya mizigo zitakazosaidia usafirishaji wa bidhaa zetu hasa zile za kuharibika haraka ikiwemo mazao ya mashambani kwenda nje ya nchi, "Mpaka sasa tuna ndege 13 ambazo zinamilikiwa na shirika la ndege la Tanzania," alisema.
Wakati akijibu maswali kutoka kwa wananchi na waandishi RC Chalamila aligusia suala la bandari ambapo amefafanua uwekezaji uliofanywa ni mkubwa na utatuletea manufaa ni wajibu wetu kuendelea kumuunga mkono Mhe Raisi Dkt Samia.
Naye msemaji mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi alimshukuru mkuu wa mkoa wa DSM kwa maandalizi ya mkutano huu na kutoa rai kwa wanahabari kwamba waandike habari za kimaendeleo kama ilivyokuwa kipindi cha baba wa taifa Hayati Julias K. Nyerere alivyotuasa hali itakayopelekea wananchi kupata hatari kujua nini Serikali inawafanyia katika sekta na maeneo mbalimbali.
Sambamba na hilo pia wakurugenzi wote kutoka mkoa wa DSM walielezea kiufupi mafanikio waliyoyapata kwenye majiji yao na kupongeza juhudi zinazofanywa na awamu hii wakieleza 'mambo ni mengi ila muda ni mchache' kuelezea yote, Mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu inayosema #TumewasikiaTumewafikia ambapo wakuu wote wa mikoa ya Tanzania bara watakutana na wakurugenzi wao kujadili mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwenye mikoa yao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa