Uzinduzi wa Utoaji Zawadi za Rais SSH,20.12.2022 katika kituo cha Hisani Orphanage Center Kigamboni-DSM
-Waziri Dkt Dorothy Gwajima akabidhi zawadi hizo kuashiria Uzinduzi rasmi wa Utoaji wa zawadi hizo katika Mikoa yote ya Tanzania Bara
-Watoto wenye Uhitaji katika kituo cha Hisani Orphanage Center wamshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe Dkt Dorothy Gwajima leo amekabidhi zawadi za sikukuu za mwisho wa mwaka zilizotolewa na Rais *Mhe Dkt Samia Suluhu katika kituo cha Kulelea watoto wenye mahitaji maalum kinachoitwa Hisani Orphanage Center Kigamboni-Dar es Salaam.
Mhe Dkt Dorothy Gwajima amekabidhi zawadi mbalimbali katika kituo hicho ikiwemo Mchele, Juice, Mafuta ya kupikia, Maharage, Chunvi na Mbuzi wawili (2)
Akikabidhi Zawadi hizo Mhe Dkt Dorothy Gwajima amesema Rais Samia anawapenda sana ametoa zawadi hizo ikiwa ni salamu maalum kutoka kwake kwa niaba ya vituo takribani 29 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara, Utoaji wa zawadi hizo katika kituo hicho ni Uzinduzi rasmi ambapo kuanzia tarehe 22-24 Disemba wakuu wa Mikoa kwa kushirikiana na wadau wengine watakao guswa na watu wenye uhitaji wataendelea kutoa zawadi hizo katika maeneo yao au Mikoa yao.
Aidha Waziri amefurahishwa na namna kituo hicho kinavyotoa malezi bora ambapo kwa sasa kituo kinalea watoto zaidi ya 60" Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anatoa wito na hamasa kwa watanzania wote wenye upendo kote nchini kuungana naye kuendelea kuwakumbuka wenye uhitaji tunapoadhimisha Sikuu za mwisho wa mwaka 2022 na mwaka mpya 2023 na anawatakia heri ya Sikukuu" Alisema Waziri Dkt Dorothy Gwajima
Hata hivyo watoto wenye uhitaji katika kituo hicho wamshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu kwa Upendo wake kwao na wanamuombea kwa mwenyezi Mungu maisha marefu ili aendelee kuwatumikia
Ifahamike kuwa hivi sasa nchini Tanzania kuna jumla ya Watoto 9011 ( Me 4897 na KE 4114) wanaopata huduma za msingi katika makao ya Watoto 325 yaliyosajiliwa yakiwemo 2 ya Serikali aidha Jumla ya Wazee Wasiojiweza ni 263 ( Ke 159 na KE 104) wanaohudumiwa Kwenye makazi 14 ya Serikali na wengine 537 ( Me 278 na KE 259) kwenye makazi ya watu binafsi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa